Wanariadha,timu za michezo pamoja na mashabiki kutoka pembe zote za ulimwengu wameanza kuwasili mjini Rio de Janeiro,Brazil kabla ya kufunguliwa kwa michezo ya Olimpiki ya 2016, siku ya Ijumaa.
Michezo hiyo imekumbwa na utata kuhusu kusitishwa kwa Russia baada ya kasfa ya utumizi wa madawa ya kusisimua misuli pamoja na madai ya dhuluma kutoka kwa makundi ya kutetea haki za kibinaamu. Ufukwe wa Ipanema umefurika wageni tangu mwanzo wa juma hili.