Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 13:26

Riek Machar awasili Juba


Bango katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba April 15, 2016 likimuonyesh Rais Salva Kiir na kiongozi wa uasi, Riek Machar.
Bango katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba April 15, 2016 likimuonyesh Rais Salva Kiir na kiongozi wa uasi, Riek Machar.

Kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini, Riek Machar, amewasili mjini Juba hivi leo baada ya safari yake kuakhirishwa mara kadhaa jambo ambalo limedumaza utaratibu wa Amani ili kumaliza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yalioikumba nchi hiyo.

Watu mashuhuri wamekusanyika kwenye uwanja wa ndege mjini Juba wakisubiri kuwasili kwa Machar ikiwa ni mara ya kwanza tangu kuzuka mapigano 2013.

Machar anatarajiwa kuapishwa kuwa makamu wa rais mara tu baada ya kuwasili na kuanza kuunda serikali ya muungano kwa ushirikiano na Rais Salva Kirr. Mizozo juu ya idadi ya wanajeshi na aina ya silaha anazoruhusiwa kubeba kwenye kikosi chake kumechelewesha kurejea kwake mjini Juba. Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema Jumatatu kuwa wangetaka kuona Machar akirejea Juba haraka iwezekanavyo kama juhudi ya kuleta Amani nchini humo.

XS
SM
MD
LG