Makamu rais wa kwanza wa zamani nchini Sudan Kusini aliyopo uhamishoni na pia kiongozi wa kundi la Sudan People Liberation Movement In Opposition, SPLM-IO, Riek Machar, amesema viongozi waliotia saini mkataba wa Amani wa Agosti mwaka jana katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, wanatakiwa kuitisha mkutano wa dharura wa vyama vya kisiasa nchini Sudan Kusini ili kuelezea hali dhoofu ya kisiasa iliyopo hivi sasa nchini humo.
Machar aliiambia Sauti ya Amerika-VOA katika mahojiano ya Alhamisi kwamba vikosi vyake haviko tayari kupambana na serikali ya Rais Salva Kiir.
Alisema kipaumbele chake ni kutekeleza mkataba wa Amani uliotiwa saini mwezi Agosti.
Aliendelea kusema kwamba kama nilikuwa na mpango wa kupigana huko Juba, ningewasubiri idadi ya wanajeshi wangu 2,910 waliopo tayari Juba.
Lakini sikusubiri hilo, kwa sababu nilitaka utekelezwaji wa mkataba wa Amani ukamilike kwanza.