Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 15:21

Janet Reno mwanasheria mkuu wa kwanza mwanamke afariki dunia


Janet Reno akila kiapo cha kushika wadhifa wa Mwanasheria Mkuu wa Marekani, Machi 12, 1993.
Janet Reno akila kiapo cha kushika wadhifa wa Mwanasheria Mkuu wa Marekani, Machi 12, 1993.

Janet Reno mwanamke wa kwanza kuhudumu kama mwanasheria mkuu wa serikali kuu ya Marekani, amefariki Jumatatu kutokana na matatizo ya ugonjwa wa Parkison. Alikuwa na umri wa miaka 78.

Alihudumu kwa takriban miaka minane chini ya utawala wa rais Bill Clinton, alianza kazi hiyo kwa kuidhinisha idara ya upelelezi ya Marekani (FBI) kuvamia Branch Davidian karibu na Waco, Texas hatua ambayo ilipelekea vifo vya watu 80 waliohusika katika mapambano marefu na maafisa wa serikali kuu.

Mwaka 2000, kwa mara nyingine tena alizungumziwa sana katika kesi ya mtoto wa kiume wa miaka sita raia wa Cuba, Elian Gonzalez ambaye mama yake alifariki akiwa na jamaa zake huko Florida.

Reno aliidhinisha mawakala wa serikali kuu kumkamata Gonzalez kusudi aweze kurejeshwa Cuba kwa baba yake. Amekuwa akijulikana kwa mtindo wa moja kwa moja na kufanya kazi kwa juhudi ya kuzungumzia upinzani mkali dhidi ya utoaji mimba na kiwango cha ghasia kinachoonyeshwa kwenye televisheni na kusababisha kufunguliwa kwa kesi dhidi ya kampuni kubwa ya kompyuta ya Microsoft.

Mwaka 1998, Reno alimpa mwendesha mashtaka maalum Kenneth Starr idhini ya kupanua uchunguzi kuhusiana na mikataba ya ardhi huko Arkansas yaliyomhusisha Clinton na kujumuisha mahusiano ya kimapenzi kati ya Clinton na mfanyakazi mwanafunzi katika ikulu ya Marekani. Juhudi hizo hatimaye zilipelekea azma ya baraza la wawakilishi kutaka kumshtaki rais kuondolewa mamlakani, ingawaje baadaye alifutiwa mashtaka hayo na baraza la senate.

Kabla ya Clinton kumteua mwanasheria mkuu, Reno aliweka historia katika jimbo la Florida kwa kuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa mwendesha mashtaka wa juu huko Miami. Mwaka 2002 alijitahidi bila mafanikio kufanya kampeni ya kuwania wadhifa wa kuwa gavana wa kwanza mwanamke katika jimbo hilo.

XS
SM
MD
LG