Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 10:20

Namna dini zinavyohifadhi maandishi ya vitabu vya dini vinapochakaa


Waislam wa Afghanistan wakisoma kitabu kitakatifu cha Quran wakati wa maadhimisho ya siku ya kuzaliwa mtume Mohammad huko Kabul, Afghanistan
Waislam wa Afghanistan wakisoma kitabu kitakatifu cha Quran wakati wa maadhimisho ya siku ya kuzaliwa mtume Mohammad huko Kabul, Afghanistan

Dini kuu tatu zina sheria tofauti juu ya namna ya kutupa nakala zilizochakaa za maandishi ya dini

Quran haitakiwi kutupwa. Wayahudi wanaweza kuzika nakala za Torah au wanahifadhi kwenye chumba maalumu. Waroman Katoliki wanaweza kuzika biblia, wakati Waprotestant hawana njia maalumu ya kufanya iwapo inatokea jambo la aina hii.

Dini kuu tatu zinazotokana na imani ya Abraham zina sheria tofauti juu ya wapi na namna maandishi yao ya dini yanaweza kuteketezwa:

  • Uislamu: Quran inaweza kuteketezwa kama kuna makosa katika maandishi au kama kitabu chenyewe kimechakaa mno. Katika hali kama hiyo, wanazuoni wanasema kuna njia mbili sahihi za kufanya hivyo, moja ni kukifunika vizuri kwa kutumia nguo na kisha kukizika au kuosha karatasi zenye maandishi ya Quran kwa maji au kutupa baharini
  • Roman Catholic: Wakatoliki wanaweza kuzika biblia pale inapohitajika kufanywa hivyo, japokuwa kulikuwa na matukio katika karne za tano hadi 15 kwa ambapo biblia iliteketezwa kwa moto kama kutoa zaka.
  • Protestanti: Waprostanti hawana njia maalumu kuhusu namna ya kutupa maandishi ya dini.
  • Uyahudi: Kwa wayahudu neno lolote linaloingiza jina la mungu linatakiwa lizikwe pale ambapo maandishi hayo hayatumiki tena, au kuweka katika chumba maalumu chenye kupewa hadhi kijulikanacho kama “Geniza”. Eneo la makaburi ya wayahudi mara nyingi linakuwa na makaburi kwa ajili ya maandishi ya dini. Baadhi ya viongozi wa kiyahudi wa nchini Marekani hivi karibuni walieleza kwamba inafaa kwa vitabu vya dini kurejeshwa viwandani na kutumiwa kutengeneza upya karatasi..

Maandishi ya dini – yale yanayotokana na maandishi yanayoaminika kutoka kwa neno la Mungu, yana sheria tofauti juu ya wapi na namna ya kutupa maandishi hayo yanapochakaa. Lakini kile kilichopo kwa wote ni heshima inayoonekana kwenye maandishi hayo, namna ya kutumia kitabu huku ukikishika kama vile kukibusu kitabu hicho ukiwa umekishikilia kwa mikono miwili au kuweka kitabu kingine juu yake.

Nchini Afghanistan, ghasia zilizosababisha mauaji zilitokea baada ya jeshi la Marekani kuteketeza nakala kadhaa za Quran kwa kuzichoma moto.

XS
SM
MD
LG