Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 08:47

REG yaichapa US Monastir


Jean Jacques wa REG akikimbia na mpira wakati wa mchezo dhidi ya Union Sportive Monastirienne Machi 14, 2022.(Picha na Pape Emir/NBAE kupitia Getty Images).
Jean Jacques wa REG akikimbia na mpira wakati wa mchezo dhidi ya Union Sportive Monastirienne Machi 14, 2022.(Picha na Pape Emir/NBAE kupitia Getty Images).

Timu ya Rwanda (REG) imepata ushindi dhidi ya timu inayoongoza ya US Monastir ya Tunisia kwa kichapo cha pointi 77-74 katika kanda ya Sahara katoka ligi ya mpira wa Kikapu barani Afrika kwenye Uwanja wa Dakar Arena Jumatatu

REGG ilikuwa nyuma mapema lakini Walker akawasogeza karibu katikati ya kipindi cha kwanza baada ya pasi kutoka kwa Filer

Majok alichukua mpira wa rebaundi baada ya kukosa kwa Ghayaza na kupachika mpira nyavuni.

Filer anapiga pointi tatu nyingine na REG wanakuwa karibu ya wapinzani wao katika kota ya tatu.

Pointi tatu nyingine tatu za Moyo baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Filer zinaiweka REG pointi moja mbele ya Monastir na kumaliza kota ya tatu.

Dixon wa Monastir alikuwa na jibu la haraka na kwa kupachika pointi tatu na kuweka pointi za timu hizo karibu.

Manga anaendeleza uongozi wa REG kwa kuweka ndani pointi moja na kufuatiwa na kupachika pointi nyingine baadaye.

Slimane wa Monastir anaiweka timu yake karibnu kwa kupachika pointi nyingine.

Filer anapachika poiti moja kati ya mbili za mpira wa faulo na kuiweka REG mbele na hatimaye kuibuka na ushindi wa poiti 77-74.

XS
SM
MD
LG