Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 03:35

Rawlings:Viongozi wa Afrika wahukumiwe Afrika, sio ICC


Rais wa zamani wa Ghana, Jerry John Rawlings
Rais wa zamani wa Ghana, Jerry John Rawlings

Viongozi wa Afrika wanaoshutumiwa kwa uhalifu wa vita nchini mwao wahukumiwe ndani ya nchi zao

Rais wa zamani wa Ghana Jerry Rawlings anasema nchi za Afrika na sio mahakama ya kimataifa inayoshughulika na uhalifu-ICC- iwahukumu viongozi wa Afrika walioshutumiwa kwa uhalifu wa vita.

Bwana Rawlings ambaye hivi sasa ni mwakilishi wa Umoja wa Afrika-AU alitoa matamshi hayo Jumatatu kwenye kikao cha ufunguzi cha bunge la umoja wa nchi za kiafrika katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.

Rais wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo na baadhi ya wanasiasa maarufu nchini Kenya ni miongoni mwa watu waliofunguliwa kesi za uhalifu wa vita katika mahakama ya ICC, yenye makao yake the Hague.

Serikali mpya nchini Libya na ICC wanabishana juu ya iwapo Libya ina uwezo wa kuendesha kesi kwa usawa dhidi ya Saif al-Islam Gadhafi, mtoto wa kiume wa marehemu kiongozi wa zamani nchini Libya, Moammar Gadhafi. Bwana Rawlings alielezea kuiunga mkono Libya.

“Kama walibya walionekana wanastahiki na walishinda kuuangusha utawala wa Gadhafi katika nia yao ya kutaka uhuru na sheria, kwa nini wakati huu hawastahiki na hawana uwezo wa kutosha kuwahukumu watu wao wenyewe?”

Matamshi yake yamekuja wiki moja kabla ya ICC kuelezea juu ya hatma ya kesi dhidi ya raia sita wa Kenya iwapo watafunguliwa mashtaka au la. Wakenya hao ambao ni pamoja na naibu Waziri Mkuu nchini humo wanashutumiwa kwa kupanga matukio ya ghasia za kikabila baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 uliokuwa na utata ambao ulisababisha vifo vya watu 1,300.

XS
SM
MD
LG