Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 08:38

Raundi ya 16 ya AFCON yapangika


Mchezaji wa Zimbabwe Khama Billiat, kushoto, akifunga goli la kifungua dimba wakati timu ya Uganda na Zimbabwe katika kundi A zilipopambana katika michuano ya AFCON, Jumatano, Juni 26, 2019. (AP Photo/Hassan Ammar)
Mchezaji wa Zimbabwe Khama Billiat, kushoto, akifunga goli la kifungua dimba wakati timu ya Uganda na Zimbabwe katika kundi A zilipopambana katika michuano ya AFCON, Jumatano, Juni 26, 2019. (AP Photo/Hassan Ammar)

Raundi ya pili ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika, AFCON, itaanza Ijumaa baada ya kumalizika kwa raundi ya kwanza Jumanne na timu 16 kufuzu raundi ya pili zikiongozwa na wenyeji Misri.

Mechi za kwanza Ijumaa zitakuwa baina ya wawakilishi pekee wa Afrika Mashariki, Uganda, dhidi ya Senegal katika uwanja wa Cairo International. Pambano jingine siku hiyo litakuwa baina ya Morocco na Benin katika uwanja wa Al- Salaam mjini Cairo.

Katika raundi hiyo ya pili ambayo itakuwa katika mtindo wa mtoano wenyeji Misri watachuana na Afrika Kusini, DRC itapambana na Madagascar timu ambayo ilikuwa "Cinderella" wa fainali hizi, timu ambayo imeingia katika fainali hizo kwa mara ya kwanza na kushinda kundi lake kwa pointi saba ikiwa ni pamoja na kuifunga timu ngumu ya Nigeria 2-0 katika raundi ya kwanza.

Mechi nyingine za raundi ya pili ni Ghana dhidi ya Tunisia, Mali na Ivory Coast, Algeria dhidi ya Guinea na Nigeria itapambana na Cameroon katika moja ya mechi inayotazamiwa kuwa kali katika raundi ya pili.

Timu za Afrika Mashariki, Tanzania na Burundi zilimaliza mashindano kwa kufungwa mechi zote tatu wakati Kenya ilishinda mechi moja dhidi ya Tanzania na kufungwa na Senegal na Algeria.

Robo fainali za mashindano haya zitaanza Julai 10 na nusu fainali zitakuwa Julai 14 wakati mechi ya fainali ya mwisho itachezwa Julai 19.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC

XS
SM
MD
LG