Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 09, 2023 Local time: 10:02

Rais Blaise Compaore ajiuzulu


Mkuu wa majeshi amechukua madaraka ya kuiongoza Burkina Faso baada aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Blaise Compaore kujiuzulu.

Jenerali Honore Traore aliwaambia wana habari mjini Ouagadougou mapema leo kwamba yeye ndiye mkuu wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi kwa sasa.

Generali huyo aliya-anza madaraka hayo jana, pale alipotangaza mipango ya serikali ya mpito na kuamrisha watu kukaa majumbani baada ya ghasia za waandamanaji kwenye makao makuu ya serikali dhidi ya Bwana Compaore.

Vyombo vya habari vya Burkina Faso vilitangaza taarifa ambayo Bwana Compaore alitangaza siku 90 za mpito kuelekea uchaguzi. Wakoloni wa zamani wa nchi hiyo Ufaransa, kwa haraka wamesema wamepokea kujuizulu kwake.

Televisheni ya “Burkina 24” imetangaza kwamba Rais huyo wa zamani aliondoka kutoka ikuli chini ya ulinzi mkubwa. Bwana Compaore ameoiongoza Burkina Faso kwa kipindi cha miaka 27 baada ya kupinduliwa na kuuliwa kiongozi mpenda mageuzi na maendeleo Thomas Sankara.

XS
SM
MD
LG