Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 28, 2023 Local time: 23:06

Rapper 50 cent asikitishwa na hali ya wakimbizi Somalia


Wakimbizi walio kambini huko Somalia kwenye kambi.
Wakimbizi walio kambini huko Somalia kwenye kambi.

Rapper 50 cent asikitishwa na hali ya wakimbizi Somalia

Nyota wa muziki wa Rap Marekani Curtis Jackson anayejulikana kwa mashabiki kama 50 cent ameyaita maeneo ya kambi za wakimbizi Somalia kuwa ni ya kusikitisha.

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa mataifa hivi karibuni lilimpeleka Jackson kwenye ziara Somalia na Kenya ili aweze kujionea mapambano dhidi ya njaa katika pembe ya Afrika.

Jackson alizungumza jana kuhusu ziara yake katika eneo la Kambi ya Kabasa katika mkoa wa kusini mwa Somalia wa Dolow, ambapo maelfu wamekimbilia kupata hifadhi kutokana na njaa na vita. Jackson amesema wanawake na watoto wametoa kila kitu ili tu waweze kupata chakula.

XS
SM
MD
LG