Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 20, 2023 Local time: 19:48

Rapa wa Afrika Kusini Costa Titch afariki dunia akiwa jukwaani

Rapa wa Afrika Kusini Costa Titch anaonekana kwenye picha iliyowekwa kwenye Twitter yake Desemba 21, 2022.

Rapa wa Afrika Kusini Costa Titch alifariki dunia akiwa jukwaani alipokuwa akitumbuiza, polisi walisema Jumapili, walipofungua uchunguzi kuhusu mazingira ya kifo cha ghafla cha kijana huyo mwenye umri wa miaka 28.

Msanii huyo alianguka alipokuwa akitumbuiza Jumamosi jioni kwenye tamasha la Ultra huko Afrika Kusini katika kitongoji cha Johannesburg cha Nasrec, polisi waliambia AFP.

Walisema uchunguzi utabainisha chanzo cha kifo hicho.

Costa Titch alitamba na kibao chake maarufu Big Flexa ambacho kimetazamwa zaidi ya mara milioni 45 kwenye YouTube, akionyesha aina ya muziki wa Amapiano muziki wakwao unaojumuisha house, jazz na muziki wa maeneo ya Lounge.

Video kwenye mitandao ya kijamii za tamasha lake Jumamosi zinamuonyesha akicheza na kipaza sauti chake mkononi anapoonekana kuanguka halafu anaendelea kuimba lakini anaanguka tena, na kusababisha wasanii wengine kumsaidia.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG