Chama tawala nchini Afrika Kusini cha ANC kitashinda wingi wa kura katika uchaguzi wa mwaka 2024 na hakitahitaji ushirika ili kutawala, Rais Cyril Ramaphosa alisema hayo siku ya Jumamosi, licha ya kuwa na changamoto katika kura za maoni.
ANC itapata wingi wa kutosha tuna imani tutaibuka washindi alisema rais huyo wa African National Congress (ANC).
Tangu mwisho wa enzi ya ubaguzi wa rangi mwaka 1994 ANC ambayo ilipambana na utawala wazungu walio wachache, imemchagua mkuu wa nchi huko Afrika Kusini.
Mwaka ujao Waafrika Kusini watachagua wabunge, na mwisho wa upigaji kura, ni chama chenye wabunge wengi ndio kinamteua rais.
Forum