Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 22:49

Ramaphosa awasihi wakaazi nchini Afrika kusini kupata chanjo ya COVID-19


Rais wa Afrika kusini, Cyril Ramaphosa
Rais wa Afrika kusini, Cyril Ramaphosa

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika kusini alisema nchi hiyo sasa ina vifaa vya kutosha vya chanjo, chanjo ni muhimu kwa ajili ya kufufua uchumi wetu kwa sababu watu wengi zaidi wanavyochanjwa maeneo mengi ya shughuli za kiuchumi yatafunguliwa

Afrika kusini inatayarisha hospitali zake kwa ajili ya kulaza wagonjwa zaidi wakati aina mpya ya kirusi cha corona cha Omicron kinaisukuma nchi hiyo katika wimbi la nne la kesi za COVID-19, Rais Cyril Ramaphosa alisema Jumatatu.

Kirusi cha Omicron kiligunduliwa kwa mara ya kwanza kusini mwa Afrika mwezi uliopita na kimezua taharuki ulimwenguni huku serikali zikihofia ongezeko jingine la maambukizi. Maambukizi ya kila siku Afrika kusini yaliongezeka wiki iliyopita, hadi zaidi ya kesi 16,000 siku ya Ijumaa kutoka takribani kesi 2,300 siku ya Jumatatu.

Ramaphosa alisema katika gazeti la kila wiki kwamba kirusi cha Omicron kinaonekana kutawala katika kesi mpya kwenye majimbo mengi nchini humo ambayo jumla ni tisa na kuwasihi watu wengi kupata chanjo dhidi ya COVID-19.

Afrika kusini sasa ina vifaa vya kutosha vya chanjo, chanjo ni muhimu kwa ajili ya kufufua uchumi wetu kwa sababu watu wengi zaidi wanavyochanjwa maeneo mengi ya shughuli za kiuchumi yatafunguliwa, alisema.

XS
SM
MD
LG