Akipokea ripoti ya uchunguzi huo, Rais Cyril Ramaphosa ameielezea rushwa kama “shambulio kwa demokrasia ya nchi.”
Ripoti hiyo imekabidhiwa kwa Ramaphosa kwenye ofisi yake mjini Pretoria na kiongozi wa jopo la uchunguzi na mwanasheria mkuu, Raymond Zondo, katika hafla iliyopeperushwa kwenye televisheni.
Uporaji na usimamizi mbovu wa mashirika ya serikali ya Afrika Kusini wakati wa miaka tisa ya Zuma madarakani umepewa jina la “utekaji wa serikali.”
“Ripoti hii inatupa fursa ya kuchukua hatua madhubuti kumaliza enzi ya utekaji wa serikali,” amesema Ramaphosa.
“Utekaji wa serikali hakika ulikuwa shambulio kwa demokrasia yetu. Unavunja haki ya kila mwanaume, kila mwanamke na kila mtoto nchini humu.”