Ramaphosa amezungumzia hatua ambazo zimechukuliwa na serikali kusaidia watu kufuatia mafuriko hayo, pamoja na ufadhili zaidi baada ya kutangaza mafuriko hayo kuwa janga la kitaifa.
Kuna sehemu nyingi zilizoathiriwa na maafuriko hayo, ambazo hazijapata msaada kutoka kwa serikali.
Rais Ramaphosa amesema kwamba zaidi ya dola milioni 63 zimetengwa kwa ajili ya msaada kufuatia mafuriko hayo, na kwamba msaada zaidi wa kifedha utatolewa kupitia mchakato wa bunge.
Kamati maalum ya bunge inatarajiwa kuundwa kusimamia utoaji wa msaada huo.
Timu maalum ya Umoja wa mataifa imewasili KwaZulu Natal, kwa ziara ya siku tatu kuthathmini uharibifu uliotokea.