Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 24, 2024 Local time: 03:20

Ramaphosa ahojiwa na wabunge kuhusu wizi wa fedha kwenye shamba lake


Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa
Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa

Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa Jumanne amekabiliwa na maswali makali bungeni, wakati wabunge  walipotaka  majibu jinsi anavyokabiliana na wizi wa  mamilioni ya dola kutoka kwenye shamba lake.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP Ramaphosa alipigiwa kelele na wabunge wa upinzani wakimtaka ajibu maswali kuhusu wizi kwenye shamba lake la Phala Phala lililopo katika jimbo la Limpopo. Hata hivyo kikao cha bunge kilisitishwa kabla ya kiongozi huyo kujibu maswali.

Ramaphosa anachunguzwa kutokana na madai kwamba alikuwa na fedha za kigeni shambani kwake ambazo hazikufichuliwa kwa maafisa wa fedha, hali iliyoleta mashaka kwa wabunge wanaodai kwamba alikataa kufuatilia wizi wa fedha hizo kutokana na kuwa alikuwa amezihifadhi kinyume cha sheria.

Ramaphosa baada ya kuulizwa maswali alisema kwamba ameshauriwa dhidi ya kutoa matamshi ya umma kuhusu suala hilo hadi pale uchunguzi utakapo kamilika. Hata hivyo baadhi ya wabunge wa upinzani walisema kwamba alihitajika kujibu, kwa kuwa wizi huo bado haujafikishwa mbele ya mahakama.

XS
SM
MD
LG