Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 25, 2024 Local time: 20:12

Rais Zelenskyy aapa kuiwajibisha Russia kwa mauaji ya Ukraine


Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, katika hotuba yake ya kila siku  Jumamosi amesema kwamba Russia imekuwa mbadala wa ugaidi, na itakuwa mfano baada ya kushindwa na kupata adhabu inayo stahili kwa ugaidi wake.

Zelenskyy amesema, mashambulizi ya Russia ya Jumamosi yamechukua maisha ya watu huko Kherson ambao walikuwa wamekwenda dukani kufuata mahitaji yao.

Katika shambulizi hilo raia watatu wa Ukraine walifariki dunia. Tangazo la vikwazo limechapishwa, amesema Zelenskyy, ambapo zaidi ya makampuni 280, na watu 120 ambao walikuwa wanaendesha biashara ya kamari na kukabiliana na Ukraine, walitoa fedha kutoka serekalini na kufadhili mikakati ya Russia.

Wizara ya ulinzi ya Uingereza imesema Jumamosi kupitia taarifa zake za kijasusi kuhusu Ukraine, kwamba Russia imepata athari ya vifo vingi katika vita hivyo.

XS
SM
MD
LG