Rais Zelenskyy amesema hayo katika hotuba yake kwa taifa ya kila siku Jumamosi usiku, na kuongeza kwamba Russia itashindwa kikamilifu kwa uhakika uliopo dhidi ya uvamizi wake na mgogoro kiujumla.
Amesema Ukraine haijapokea mpango wowote wa upatanishi kutoka China ama wa kukutana na rais wa China, Xi Jingping, rais Zelenskyy aliliambia shirika la habari la Japan News.
Mkuu wa shirika la kimataifa la usimamizi wa nguvu za Atomiki la Umoja wa Mataifa, Rafael Grissi, atatembelea kituo cha nguvu za nyuklia cha Zaporizhzia, mashariki mwa Ukraine wiki ijayo kufanya tathimini ya hali kamili ya usalama kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.