Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 08, 2024 Local time: 15:02

Rais wa china awasihi viongozi wa Afrika kutumia zaidi bidhaa za Kichina


Rais wa China Xi Jinping akiwa na viongozi wa Afrika kabla ya ufunguzi wa Kongamano huko Beijing Septemba 5, 2024. Picha na Andy Wong / POOL / AFP
Rais wa China Xi Jinping akiwa na viongozi wa Afrika kabla ya ufunguzi wa Kongamano huko Beijing Septemba 5, 2024. Picha na Andy Wong / POOL / AFP

Rais wa China Xi Jinping awasihi viongozi wa Afrika Kiafrika kutumia bidhaa zaidi za Kichina kwa mabadilishano ya ahadi ya mikopo na uwekezaji

Wakati wa ufunguzi wa kikao hicho cha tisa cha Kongamano la Ushirikiano kati ya China na Afrika Alhamisi, Xi alikuwa mwenyeji wa zaidi ya dazeni mbili ya viongozi wa Kiafrika katika dhifa ya kitaifa mjini Beijing siku ya Jumatano.

Jinping aliuanzisha rasmi mkutano huo mkubwa wa viongozi katika miaka kadhaa huku kukiwa na ahadi za ushirikiano katika miundo mbinu, nishati na elimu.

China, ambayo ni ya pili kwa uchumi mkubwa duniani, ni mshirika mkubwa wa biashara na Afrika inataka kupata rasilimali nyingi katika bara hilo ikiwemo shaba, dhahabu, lithium na madini adimu yaliyopo kote katika ardhi.

Viongozi wa Kiafrika watakuwa wanatazamia masuluhisho ya haraka ya ufadhili kwa mzozo wa kuongezeka kwa deni kote katika bara hilo katika Beijing Action Plan y.a Mkutano wa Ushirikiano wa China na Afrika kwa mwaka 2025 na 2027, pamoja na ahadi za uwekezaji na uhakikisho wa miradi iliyopendekezwa Dakar inakamilishwa.

Rais Xi Jinping wa China akipiana mkoni na rais wa Senega Bassirou Diomaye Faye
Rais Xi Jinping wa China akipiana mkoni na rais wa Senega Bassirou Diomaye Faye

Viongozi 25 wa Afrika wamewasili Beijing katika mkutano wa wiki hii wa China na Afrika, ikiwa ni pamoja na baadhi ya nchi ambazo zinakabiliwa na hatari kubwa ya madeni.

Juu juu unaona ni tabasamu na kupeana mikono huko Beijing, wakati viongozi wa Afrika wakikusanyika kwa mkutano mkubwa wa mara ya tatu kwa mwaka. Lakini huenda kukawepo mazungumzo mazito hapo mbele – wakati azma ya nchi za bara hilo ni kusimama dhidi ya vipaumbele vipya vya China ambavyo vimepunguzwa.

Akiongea na waandishi wa habari Chen Xiaodong, Makamu Waziri wa Mambo ya Nje, amesema wakati wa mkutano wa FOCAC, mikutano minne ya ngazi ya juu itafanyika sambamba.

“Mada za mikutano hii zitajumuisha ‘utawala wa nchi,’ ‘viwanda na kilimo cha kisasa,’ ‘amani na usalama’ na ‘ushirikiano wa ubora wa Miundo Mbinu.’ Mada hizi nne zinaonyesha wazi ujumbe na mahitaji ya wakati wetu, na kukumbatia wasi wasi wa kawaida na matarajio ya China na Afrika kwa hali ya kisasa, na pia ni kiini kwa mwelekeo kwa mkutano kusonga mbele katika enzi mpya.” Alisema Xiaodong.

Rais Xi Jinping akipeana mkono na rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa
Rais Xi Jinping akipeana mkono na rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa

Aliongeza Makamu Waziri wa Mambo ya Nje, kwamba mikutano pia itatoa muda zaidi kwa pande zote kufanya mabadilishano ya kina kwa masuala muhimu sana na shinikizo katika ushirikiano wa China na Afrika, wakati wakiimarisha dhana ya mawasiliano, kujenga maelewano juu ya maendeleo, na kuongeza uhai katika ujenzi wa pamoja wa ngazi ya juu wa China na Afrika wenye mustakbali wa pamoja.

Lakini mchambuzi wa Afrika anahoji kama Waafrika kwa kweli wananufaika na aina hii ya uhusiano. Bravious Kaihoza ni mchumi wa jijini Dar es Salaam anasema uhusiano na biashara kati ya pande mbili umeboreka sana lakini kwa kiwango fulani waafrika hawajanufaika.

Mkutano wa China na AFrika ambao utafikia kilele kesho Ijumaa unatarajiwa kumalizika kwa viongozi wengi wa kiafrika kuingia katika mikataba mbali mbali na China kwa ajili ya uhusiano wa kibiashara na bara hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG