Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 13, 2025 Local time: 14:24

Liberia: Rais Weah na kiongozi wa upinzani Boakai wanakaribiana katika matokeo ya awali


Rais wa Liberia aliyepo madarakani George Weah (kulia) na mpinzani wake mkuu Joseph Boakai. Picha na JOEL SAGET na Brendan SMIALOWSKI / AFP.
Rais wa Liberia aliyepo madarakani George Weah (kulia) na mpinzani wake mkuu Joseph Boakai. Picha na JOEL SAGET na Brendan SMIALOWSKI / AFP.

Rais wa Liberia George Weah na kiongozi wa upinzani Joseph Boakai wanakaribiana katika matokeo wakiwa katika kinyang’anyiro cha urais.

Matokeo ya awali jana Jumapili (Oktoba 15) yalionyesha kuwa Weah anaongoza kwa kura chache akiwa na kura asilimia 43.80, tume ya uchaguzi ilisema,

Hiyo ni kulingana na majumuisho ya matokeo kutoka takriban robo tatu ya vituo vya kupiga kura.

Makamu wa Rais wa zamani Boakai alikuwa na asilimia 43.54 ya kura.

Ikiwa hakuna hata mmoja atakayepata asilimia 50 ya kura uchaguzi utaelekea katika duru ya pili.

Weah nyota wa mpira wa miguu anayependwa na wananchi ambaye alitokea katika makazi duni ya Monrovia na kufikia kucheze katika baadhi ya klabu kubwa za kandanda duniani.

Wananchi wajitokeza kupiga kura Liberia.
Wananchi wajitokeza kupiga kura Liberia.

Lakini wakosoaji wanasema ameshindwa kuzuia ufisadi au kutatua hali ngumu ya kiuchumi inayoipitia Liberia katika miaka yake ya kwanza sita.

Weah, ambaye amejenga mahospitali na kuanzisha elimu bila malipo, anasema mgogoro wa afya duniani ulirejesha nyuma mipango yake.

Boakai anadai kuwa anahitaji kuiokoa Liberia kutokana na kile alichokiita utawala mbaya chini ya Weah.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG