Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 07:05

Rais wa Zambia aaga dunia


Rais wa Zambia Michael Sata (Katikati)
Rais wa Zambia Michael Sata (Katikati)

Waziri katika serikali Roland Msisika alithibitisha kifo chake leo Jumatano akisema kuwa bwana Sata aliaga dunia Jumanne jioni.

Rais wa Zambia Michael Sata ameaga dunia akiwa mjini London ambapo alikuwa anatibiwa kutokana na ugonjwa ambao hukutambulishwa. Alikuwa na umri wa miaka 77.

Waziri katika serikali Roland Msisika alithibitisha kifo chake leo Jumatano akisema kuwa bwana Sata aliaga dunia Jumanne jioni. Wiki jana ofisi ya rais ilisema ameondoka nchini ‘kufanyiwa ukaguzi wa afya’ lakini haikutoa maelezo zaidi.

Kumekuwa na wasiwasi juu ya afya yake tangu mwezi Juni wakati alipokwenda Israel kwa matibabu na kutoonekana hadharani kwa miezi mitatu.

Alishindwa pia kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwezi jana jijini New York ambapo ripoti za polisi zilisema aliugua ghafla na madaktari kumhudumia akiwa katika chumba chake cha hoteli.

Bwana Sata ameongoza Zambia tangu aliposhinda uchaguzi mwaka 2011 uliohitimisha utawala wa miaka 20 wa chama cha Movemnet for Multiparty Democracy. Ilikuwa ni mara yake ya nne kugombania urais.

XS
SM
MD
LG