Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 16, 2025 Local time: 08:55

Rais wa zamani wa Sierra Leone ashitakiwa kwa njama za mapinduzi


Rais wa zamani wa Sierra Leone akihutubia huko Kambia March 3, 2018. Picha na ISSOUF SANOGO / AFP.
Rais wa zamani wa Sierra Leone akihutubia huko Kambia March 3, 2018. Picha na ISSOUF SANOGO / AFP.

Sierra Leone siku ya Jumatano imemfungulia mashitaka ya uhaini pamoja na makosa mengine Rais wa zamani wa nchi hiyo Ernest Bai Koroma kwa kile mamlaka ilichodai jukumu lake katika jaribio la mapinduzi la Novemba 26, Mamlaka imesema.

Korona ambaye aliliongoza taifa hilo la Afrika Magharibi kuanzia 2007 hadi 2018, awali alihojiwa, mamlaka ikisema alikuwa mshukiwa rasmi katika mipango ya mapinduzi.

“Rais huyo wa zamani ameshitakiwa kwa makosa manne yakiwemo uhaini, makossa ya uhaini na kwa mashitaka mawili ya kuhifadhi,” taarifa iliyosainiwa na waziri wa habari Chernor Bah imesema.

Siku ya Jumanne Sierra Leone iliwafungulia mashitaka watu 12 kwa tuhuma za uhaini zinazohusiana na jaribio la mapinduzi akiwemo Amadu Koita, mwanajeshi wa zamani na mlinzi wa Koroma.

Koita alikuwa akifuatiliwa kwa kiasi kikubwa katika mitandao ya kijamii ambako amekuwa akiikosoa serikali ya sasa ya Rais Julius Maada Bio.

Novemba 26, washambuliaji wenye silaha walivamia ghala ya silaha kambi mbili za jeshi, magereza mawili, na vituo viwili vya polisi pamoja na kupambana na vikosi vya usalama.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG