Gbagbo ambaye alikuwa rais wa taifa hilo la Afrika Magharibi kuanzia mwaka 2000 hadi 2011, alikuwa rais wa kwanza wa zamani kukabiliwa na kesi ya uhalifu dhidi ya ubinadamu katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu mjini The Hague, na aliachiliwa mwaka 2019 baada ya kutopatikana na hatia.
Gbagbo mwenye umri wa miaka 78 hata hivyo alihukumiwa kifungo cha miaka 20 jela mwaka 2018 kwa kuhusika kwake katika uporaji wa benki. Alisamehewa mwaka 2022 lakini bado haruhusiwi kugombea wadhifa wa umma.
Chama chake cha African Peoples’-Ivory Coast (PPA-CI) kilimteua hata hivyo kama mgombea wao siku ya Ijumaa.
Katika hotuba ya zaidi ya saa moja, Gbagbo alisema atuhudumu muhula mmoja tu, na kuchukua hatua za kutokomeza ufisadi uliokithiri na kuifanya mahakama kuwa huru zaidi.
Forum