Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 03, 2024 Local time: 17:38

Rais wa zamani wa Guinea apelekwa nje ya nchi kwa matibabu


Rais wa zamani wa Guinea Alpha Conde
Rais wa zamani wa Guinea Alpha Conde

Rais wa zamani wa Guinea, Alpha Conde, ambaye alipinduliwa mwezi Septemba mwaka jana, aliondoka kwa ndege Jumatatu ili kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu kwa mujibu wa vyanzo viwili vya shirika la habari la Reuters pamoja na kingine ambacho hakikutaka kutambulishwa.

Mwezi uliopita utawala uliopindua nchi ulisema kwamba rais huyo wa zamani ataruhusiwa kusafiri kwa matibabu lakini hatoruhusiwa kukaa nje ya nchi kwa mwezi zaidi ya mmoja. Vyanzo vya karibu na Konde vimeeleza kwamba alipanda ndege majira ya saa nane mchana kwa saa za huko.

Afisa wa juu wa serekali alithibitisha kwamba kiongozi huyo wa zamani aliyeondoka kupitia mapinduzi ya mwezi Septemba amekuwa akikabiliwa na changamoto za kiafya. Mataifa jirani na Guinea pamoja na washirika wa kimataifa wamekuwa wakilalamikia mapinduzi hayo. Conde mwenye umri wa miaka 83 alikuwa madarakani kuanzia mwaka wa 2010.

XS
SM
MD
LG