Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 16:21

Rais wa zamani wa Guinea Alpha Conde ameachiliwa kutoka kifungo cha nyumbani


Nyumba iliyoshambuliwa aliokuwa akiisshi Rais wa zamani wa Guinea Alpha Conde katika jaribio la mapinduzi la mwaka 2011.
Nyumba iliyoshambuliwa aliokuwa akiisshi Rais wa zamani wa Guinea Alpha Conde katika jaribio la mapinduzi la mwaka 2011.

Rais wa zamani wa Guinea Alpha Conde ameachiliwa kutoka kifungo cha nyumbani zaidi ya miezi saba baada ya kuondolewa madarakani katika mapinduzi ya kijeshi, serikali ya mpito ilisema kwenye televisheni ya taifa siku ya Ijumaa.

Conde, mwenye umri wa miaka 84, alikuwa kizuizini tangu Septemba mwaka jana, wakati wanajeshi wa kikosi maalum walipompindua kwa madai ya kuendeleza ufisadi wa serikali.

Serikali mpya ya kijeshi ya Guinea imemruhusu Conde kupokea wageni, na mapema mwezi huu ilimruhusu kusafiri hadi Umoja wa Falme za Kiarabu kwa ajili ya kuchunguzwa afya yake.

Ataendelea kuishi katika nyumba ya familia ya mke wake katika kitongoji cha mji mkuu Conakry hadi ukarabati wa nyumba yake utakapokamilika, serikali ya mpito ilisema katika taarifa yake.

XS
SM
MD
LG