Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 16, 2021 Local time: 18:03

Rais wa zamani wa Ghana Jerry Rawlings afariki


Rais wa zamani wa Ghana Jerry Rawlings aliyeaga dunia tarehe 12 Novemba 2020.

Rais wa zamani wa Ghana Jerry Rawlings alifariki Alhamisi akiwa na umri wa miaka 73. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ikulu ya nchi hiyo.

Rawlings atakumbukwa kama kiongozi aliyeongoza mapinduzi ya kijeshi nchini humo, mara mbili na baadaye kuleta mfumo wa demokrasia kwa taifa hilo la Afrika Magharibi.

Alimng’oa mamlakani Generali Fredrick Akuffo mnamo mwaka wa 1979 wakati huo akiwa luteni wa jeshi.

Baadaye alikabidhi madaraka kwa serikali ya kidemokrasia, lakini miaka miwili baadaye, akaongoza mapinduzi ya pili ya kijeshi, akiishutumu serikali hiyo kwa ufisadi na uongozi dhaifu.

Kati ya mwaka wa 1981 ni 1993, Rawlings alitawala akiwa mwenyekiti wa baraza la uongozi wa pamoja wa kijeshi na kiraia. Mwaka wa 1992, alichaguliwa rais chini ya katiba mpya ya Ghana, na kuhudumu kwa mihula miwili, kabla ya kustaafu na kumwachia uongozi mrithi wake, Rais John Kufuor, mwaka wa 2001.

Hadi tukitayarisha ripoti hii, ikulu ya Ghana haikuwa imetoa maelezo yoyote kuhusu kilichosababisha kifo chake.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG