Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 19, 2024 Local time: 01:13

Rais wa zamani George Bush atazuru Afrika


Rais George W. Bush na Laura Bush walipotembelea Tanzania.
Rais George W. Bush na Laura Bush walipotembelea Tanzania.

Rais wa zamani wa Marekani George W. Bush atasafiri kwenda Afrika kuhimiza mipango ya kupambana na magonjwa kama vile Malaria na Ukimwi.

Rais wa zamani wa Marekani George W. Bush atasafiri kwenda Afrika mwezi ujao ili kuhimiza mipango ya kupambana na magonjwa kama vile Malaria na Ukimwi.

Rais huyo wa zamani akiwa na mke wake Laura watatembelea Tanzania, Zambia na Ethiopia kuanzia Desemba 1 hadi 5.Wakiwa Afrika rais huyo wa zamani na mama wa kwanza watatoa kipaumbele kwenye juhudi za kupambana na magonjwa hayo mawili zilizoanza wakati wa utawala wake na ambazo zinazoungwa mkono na taasisi ya George W. Bush ya mpango wa afya duniani.

Wakati wa utawala wake kati ya mwaka 2001 na 2009 , alisaidia katika uzinduzi wa mfuko wa dola bilioni 60 kupambana na Ukimwi , Malaria na kifua kikuu duniani kote. Msaada karibu wote unakwenda barani Afrika.

Rais Barack Obama ameendelea kuunga mkono mpango huo, ujulikanao kama PEPFAR au mpango wa rais wa msaada wa dharura wa kusaidia Ukimwi.Wakati akiwa barani Afrika taasisi ya rais Bush inasema Bw.na Bi. Bush watazungumzia njia mpya za kuzuia magonjwa ya saratani.

XS
SM
MD
LG