Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 23:15

Rais wa Yemen ataka waandamaanji walindwe


Mmoja wa waandamanaji wanaopinga serikali akionyesha risasi zilizofyatuliwa dhidi yao na waunga mkono wa serikali ya yemen.
Mmoja wa waandamanaji wanaopinga serikali akionyesha risasi zilizofyatuliwa dhidi yao na waunga mkono wa serikali ya yemen.

Rais wa Yemen Ali Abdullah Saleh amewataka vikosi vyake vya usalama kuwalinda waandamanaji ambao wanamtaka ajiuzulu .

Rais wa Yemen Ali Abdullah Saleh amewataka vikosi vyake vya usalama kuwalinda waandamanaji ambao wanamtaka ajiuzulu.

Shirika la habari la televisheni la Yemen, Saba news limetoa taarifa inayoeleza kwamba Bw. Saleh ameyataka majeshi ya usalama kuzuia mapigano yeyote kati ya waandamanaji wanaopinga serikali na wale wanaounga mkono.

Pia alizitaka pande zote mbili kuchukua tahadhari dhidi ya wale ambao watajaribu kuchochea waandamanaji na kuzidisha ghasia.

Kwa mara nyingine tena maelfu ya waandamanji wanaopinga serikali walimiminika katika uwanja mmoja katika mji mkuu wa Yemen San’aa.

Siku ya jumanne mtu mmoja aliuwawa na 12 kujeruhiwa wakati waandamanaji wa upinzani waliokusanyika katika chuo kikuu cha Sana’a kushambuliwa na watu walokua na bunduki na silaha nyenginezo walipojaribu kuwatawanya waandamanaji hao.

Kiasi ya wabunge saba wamejiuzulu kutoka chama tawala kulalamika dhidi ya utumiaji nguvu dhidi ya maandamano ya amani. Wabunge hao walieleza siku ya Jumatano kwamba wataunda kundi la wabunge wanaojitegemea bungeni.

XS
SM
MD
LG