Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 03:54

Rais wa Vietnam awasili Tanzania kwa ziara rasmi


Rais wa Vietnam,Truong Tan Sang, amewasili Tanzania kwa ziara ya siku tatu.
Rais wa Vietnam,Truong Tan Sang, amewasili Tanzania kwa ziara ya siku tatu.

Watanzania wametakiwa kutumia fursa ya ujio wa Rais wa Vietman, Troung Tang Sang pamoja na wafanyabiashara wa nchi hiyo kutafuta mbinu ya kutumia raslimali zilizopo nchini Tanzania kupata maendeleo ya kiuchumi.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:12 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Rais wa vietnam Trough Tang Sang pamoja na ujumbe wake wapo nchini Tanzania kwa ziara ya siku tatu yenye lengo la kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya Tanzania na Vietnam.

Rais huyo wa Vietman alipokewa rasmi ikulu jijini Dar es Salaam siku ya Jumatano na mwenyeji wake Rais wa Tanzanai John Magufuli ambaye alisisitiza rai hiyo kwa watanzania kutumia fursa ya ziara ya ujumbe wa Vietman kuinua uchumi wa Tanzania ambao mpaka sasa bado ni miongoni mwa nchi maskini duniani.

Kiongozi huyo wa Vietman aliambatana na ujumbe wa watu 51 ambao ni wafanyabishara pamoja na baadhi ya mawaziri kwenye serikali yake.

Rais wa Tanzania, John Magufuli
Rais wa Tanzania, John MagufuliRais wa Tanzania, John Magufuli na mwenzake wa Vietnam walifanya mazungumzo maalum Ikulu jijini Dar es Salaam yaliyojikita katika kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili ikiwemo kupanua wigo wa uwekezaji utakaochochea biashara kati ya Tanzania na Vietnam pamoja na kukubaliana kuwekeana mikataba ya kutowatoza kodi mara mbili wawekezaji na wafanyabishara wanaowekeza katika nchi hizi.

Bwana Sang pia atashiriki mkutano wa biashara na uwekezaji unaotarajiwa kuhudhuriwa na taasisi za umma na sekta binafsi kutoka Tanzania na Vietnam.
--------------------------------------------------------------------------------------------------

XS
SM
MD
LG