Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 15:46

Rais wa Uturuki kukutana na baraza la usalama wa taifa


Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan alitazamiwa kukutana na baraza la usalama wa taifa Jumatano asubuhi kufuatia jaribio la mapinuzi la wiki iliyopita.

Atakutana na baraza la mawaziri katika mjumuisho wa mkutano wa usalama na mara baada ya mkutano huo kunatazamiwa kutolea tangazo muhimu.

Mapema Jumatano, baraza la elimu ya juu la Uturuki lilitangaza kupiga marufuku kwa wanazuoni kusafiri nje ya nchi na kuwataka wale wote waliopo nje kurejea nchini humo haraka.

Vyombo vya habari vya Uturuki vimeripoti kwamba wizara ya elimu imewafukuza kazi waalimu 15,200 nchini kote wakati wizara ya mambo ya ndani imewafukuza wafanyakazi karibu 9,000.

Wengine 1,500 kutoka wizara ya fedha walifukuzwa huku mamia zaidi katika wizara za masuala ya kidini, familia na sera za jamii na ofisi ya waziri mkuu walifukuzwa.

XS
SM
MD
LG