Asilimia 5.2 ya kura kwa Sinan Ogan katika uchaguzi mkuu wa Mei 14 ilisaidia kumnyima Erdogan ushindi mkubwa kwa mara ya kwanza katika utawala wake wa miaka 20.
Ogan alikutana na kiongozi huyo wa Uturuki siku ya Ijumaa na kufanya mazungumzo tofauti na washirika wa kiongozi wa upinzani Kemal Kilicdaroglu.
“Tutamuunga mkono mgombea wa chama cha the People’s Alliance, Recep Tayyip Erdogan, katika duru ya pili ya uchaguzi tarehe 28 Mei, aliwaambia waandishi wa habari.
Ogan anajitambulisha kama mfuasi sugu wa mrengo wa kihafidhina wa Uturuki uliopendekezwa na muanzilishi wa jamhuri ya baada ya ufalme wa Ottoman Mustafa Kemal Ataturk.
Aliomba mamilioni ya wahamiaji wafurushwe mara moja na kupendekeza msimamo thabiti dhidi ya magaidi, neno linalotumiwa dhidi ya makundi ya Wakurdi yanayopigania uhuru eneo la kusini mashariki mwa Uturuki.