Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 29, 2023 Local time: 18:42

Rais wa Uturuki aanza ziara yake barani Afrika huko Angola


Rais Recep Tayyip Erdogan akiwa na mwenzake wa Angola João huko Luanda. Angola, Oktoba 18,2021
Rais Recep Tayyip Erdogan akiwa na mwenzake wa Angola João huko Luanda. Angola, Oktoba 18,2021

Rais Recep Tayyip Erdogan, akihitimisha ziara yake nchini Angola alihakikishia kuwa Uturuki inakusudia kukuza uhusiano na nchi za Kiafrika

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, akihitimisha ziara yake nchini Angola, ikiwa ni hatua ya kwanza ya ziara yake katika bara la Afrika alihakikishia kuwa Uturuki inakusudia kukuza uhusiano na nchi za Kiafrika kwa msingi wa ushirikiano wa makubaliano ya pande zote, katika mfumo wa kuheshimiana.

"Sisi nchini Uturuki tunaona umuhimu mkubwa na thamani kubwa kwa uhusiano wa karibu tulio nao na bara la Afrika", Rais Erdogan alisema Jumatatu jioni mbele ya hadhira ya wafanyabiashara wa Angola, kulingana na taarifa iliyotolewa na chama chake cha AKP.

Hapo awali, katika hotuba yake kwa bunge la Angola lililotangazwa kwenye tovuti ya ofisi ya rais wa Uturuki, Bwana Erdogan alieleza kwamba hatima ya ubinadamu haiwezi na haipaswi kuachwa kwa huruma ya nchi chache ambazo ni washindi wa Vita vya pili vya dunia.

Kupuuza wito wa mabadiliko ni ukosefu wa haki kwa Afrika, ameongeza, akisisitiza kwamba Uturuki haina doa la ubeberu au ukoloni.

XS
SM
MD
LG