Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 03:59

Rais wa Ufaransa yuko katika ziara ya mataifa matatu barani Afrika


Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akipokelewa na Rais wa Cameroon Paul Biya.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akipokelewa na Rais wa Cameroon Paul Biya.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, akiwa nchini Cameroon kuanza ziara yake ya mataifa 3 barani Afrika, anatarajiwa kujadili mzozo wa chakula barani Afrika uliochochewa na vita vya Russia nchini Ukraine, hitaji la Cameroon kuongeza uzalishaji wake wa kilimo.

Akiwa Yaounde, mji mkuu wa Cameroon, kwa ziara ya siku tatu katika nchi hiyo ya Afrika ya kati, Macron kisha ataitembelea Benin na Guinea Bissau.

Serikali ya Cameroon iliupa mji mkuu sura mpya kwa ziara ya Macron. Tingatinga zilibomoa vibanda vya wachuuzi na vibanda katika mitaa yote ya mjini Yaounde ambapo ujumbe wa Macron utapita.

Wameharibu chanzo changu pekee cha riziki,” alisema Solange Kemje, mwenye umri wa miaka 28, miongoni mwa mamia ya wamiliki wa vibanda walioathirikana bomoa bomoa hiyo.

Wengine walikaribisha ziara ya kiongozi huyo wa Ufaransa, wakitumai kuwa Macron atatoa msaada katika kukabiliana na ongezeko la ukosefu wa usalama kutokana na ghasia za kijihadi ambazo zimesambaa kutoka nchi jirani ya Nigeria.

Taifa hilo la Afrika ya kati pia linapambana na mzozo wa kutaka kujitenga ambao umesababisha vifo vya takriban watu 3,300 na wengine zaidi ya 750,000 kuyahama makazi yao katika kipindi cha miaka mitano, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. waasi wanawapigania watu wachache wanaozungumza lugha ya Kiingereza nchini Cameroon kuwa na nchi huru inayoitwa Ambazonia.

XS
SM
MD
LG