Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 10, 2024 Local time: 10:39

Rais wa Tunisia awaondoa mawaziri wengi


Rais wa Tunisia Kais Saied
Rais wa Tunisia Kais Saied

Rais wa Tunisia Kais Saied Jumapili alibadilisha mawaziri wengi, akiwemo wa wizara ya mambo ya nje na ulinzi, ofisi ya rais wa Tunisia ilisema katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa Facebook bila maelezo.

Mabadiliko hayo ya ghafla yamechukua nafasi ya mawaziri 19 na makatibu watatu wa serikali, siku chache tu baada ya Saied kumfukuza waziri mkuu wa zamani.

“Asubuhi Agosti 25, mwaka 2024, Rais wa Jamhuri aliamua kufanya mabadiliko ya serikali,” ilisema taarifa hiyo bila kutoa maelezo zaidi.

Hatua hiyo inajiri wakati taifa hilo la Afrika Kaskazini likijiandaa kwa uchaguzi wa rais tarehe 6 Oktoba.

Saied, mwenye umri wa miaka 66, alichaguliwa kidemokrasia mwaka 2019 lakini alijinyakulia mamlaka makubwa mwaka 2021.

Anataka kuwania muhula wa pili kama sehemu ya kile alichosema “ni vita vya ukombozi na nchi kujitegemea” vyenye lengo la kuunda jamhuri mpya.

Forum

XS
SM
MD
LG