Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 04, 2024 Local time: 17:47

Rais wa Tunisia anakosoa uingiliaji kati wa mataifa ya kigeni nchini mwake


Rais Kais Saied wa Tunisia.
Rais Kais Saied wa Tunisia.

EU na Marekani walielezea wasiwasi wao wiki hii kufuatia kukamatwa kwa waandishi, wachambuzi wa kisiasa na wanasheria.

Rais wa Tunisia Kais Saied siku ya Alhamisi alikosoa “uingiliaji kati” kwa mataifa ya kigeni baada ya upinzani wa kimataifa kuhusu kukamatwa kwa waandishi wa habari, wachambuzi wa kisiasa, na wanasheria, ambao aliutetea kama halali.

Mashirika ya kiraia katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini yamelaani kukamatwa kwa watu hao, kama ukandamizaji dhidi ya wapinzani nchini humo, ambao ulishuhudia mwanzo wa vuguvugu la mageuzi katika nchi za kiarabu-Arab Spring.

Saied ambaye alitwaa madaraka makubwa mwaka 2021, aliagiza wizara ya mambo ya nje kuwaita mabalozi wa nchi kadhaa na kuwafahamisha kuwa “Tunisia ni taifa huru”, katika video iliyotolewa na ofisi yake.

Umoja wa Ulaya umeelezea wasiwasi wake wiki hii juu ya kukamatwa kwa watu hao, wakati Marekani ikisema inapingana na haki jumla zilizosahihishwa na katiba ya nchi hiyo.

Forum

XS
SM
MD
LG