Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 13:41

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan yuko katika ziara ya kiserikali Afrika Kusini

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akiwa na Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika ziara yake ya Kiserikali kwenye Majengo ya Muungano mjini Pretoria, Afrika Kusini Machi 16, 2023.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akiwa na Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika ziara yake ya Kiserikali kwenye Majengo ya Muungano mjini Pretoria, Afrika Kusini Machi 16, 2023.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan yuko katika ziara ya kiserikali nchini Afrika Kusini akihimiza ushirikiano zaidi wa kiusalama na biashara kati ya nchi hizo mbili.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan yuko katika ziara ya kiserikali nchini Afrika Kusini akihimiza ushirikiano zaidi wa kiusalama na biashara kati ya nchi hizo mbili.

Samia Suluhu, kiongozi wa kwanza mwanamke wa Tanzania, alikutana na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa katika mji mkuu wa Pretoria siku ya Alhamisi ambapo ujumbe wake wa Baraza la Mawaziri ulijadili fursa za biashara na makubaliano yanayowezekana na wenzao wa Afrika Kusini.

Hii ni ziara ya kwanza rasmi ya Rais Samia nchini Afrika Kusini tangu awe rais wa Tanzania kufuatia kifo cha mtangulizi wake John Magufuli mwaka 2021.

"Tumekubaliana kuimarisha ushirikiano wetu katika maeneo ya biashara na uwekezaji ikizingatiwa kuwa Afrika Kusini ni miongoni mwa vyanzo vikuu vya uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni nchini Tanzania," alisema Rais Samia. Aliongeza kuwa utalii na viwanda ni sekta zinazoongoza kwa uwekezaji.

Ramaphosa alisema kiwango cha biashara kati ya Tanzania na Afrika Kusini kinaendelea kuongezeka lakini kinaweza kuboreshwa zaidi.

XS
SM
MD
LG