Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 04:30

Rais wa Sudan Kusini anasema yupo tayari kufanya kazi na upinzani


rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir
rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir

Rais Salva Kiir alisema atatumia rasilimali zote zilizo kwenye mhimili wake kuleta amani na uthabiti na alitoa wito kwa vyama vyote kufanya kazi pamoja kurejesha amani na kuruhusu watu kutembea huru kwenye maeneo ya Sudan Kusini

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir aliwasihi wabunge na maofisa wengine kuunga mkono utekelezaji wa mkataba wa kurejesha amani nchini humo ambao ulitiwa saini mwaka 2018.

Katika matamshi yake siku ya Jumanne, Kiir alieleza kwamba atatumia rasilimali zote zilizo kwenye mhimili wake kuleta amani na uthabiti. Wakati wa kufunguliwa tena bunge la muda la kitaifa la Sudan Kusini mjini Juba, Rais Kiir alionya kwamba nchi haitasonga mbele hadi serikali na upinzani waweke kipaumbele utekelezaji wa mkataba.

Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini
Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini

Alitoa wito kwa vyama vyote kufanya kazi pamoja kurejesha amani na kuruhusu watu kutembea huru kwenye maeneo. Kiir aliendelea kusema “nchi yetu ipo njia panda. Ninasimamia amani na uthabiti na ninakataa kabisa vita. Serikali yangu kwa kutambua hilo inatumia rasilimali zote kwa mamlaka yake kwa sababu ya kuelezea amani na uthabiti katika mila zetu na jukumu la dini la kuleta amani kwa watu wetu.

Kiir alipigiwa makofi kutoka kwa wabunge, wanadiplomasia na maafisa wengine waliokuwepo wakati aliposema kwamba yupo tayari kufanya kazi na makundi ya upinzani kurejesha uthabiti wa Sudan Kusini.

XS
SM
MD
LG