Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 28, 2023 Local time: 14:25

Rais wa Sudan kusini amaliza ziara Khartoum


Rais Omar al-Bashr wa Sudan (kulia) akimsikiliza mwenzake wa Sudan Kusini Salva Kiir akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi habari kabla ya Bw. Kiir kuondoka Khartoumt Oktoba 9, 2011.

Yeye na rais wa Sudan Omar al- Bashir walijadili masuala ambayo bado yanaendelea kuleta mvutano wa nchi hizo mbili.

Rais wa Sudan kusini Salva Kiir amemaliza ziara yake ya siku mbili mjini Khartoum ambako yeye na rais wa Sudan Omar al- Bashir walijadili masuala ambayo bado yanaendelea kuleta mvutano wa nchi hizo mbili.

Tatizo ambalo halijatatuliwa tangu Sudan kusini ipate uhuru wake mapema mwezi Julai ni mzozo wa eneo la Abyei lililoko kwenye mpaka lenye utajiri wa mafuta na jinsi la kushirikiana mapato ambayo yanategemewa katika mataifa hayo mawili.

Katika mkutano na waandishi wa habari jumapili viongozi wa nchi hizo walisema kamati zimeundwa katika jaribio la kumaliza mzozo ambao unachochea hofu ya kurejea tena vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Bwana Kiir alisema Serikali yake iko tayari kujadili masuala yote yaliyobaki .

Rais Bashir alisema siku ya mwisho ya suluhisho imepangwa lakini hakutoa maelezo zaidi.

XS
SM
MD
LG