Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 03, 2024 Local time: 13:06

Rais wa Somalia aapa kulitokomeza kundi la Al Shabab


Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud
Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud Jumanne ameahidi vita vikali kutokomeza kundi la Al Shabab katika taarifa yake ya kwanza kwa taifa tangu wanamgambo hao wa Kiislamu kufanya uvamizi mbaya wa saa 30 kwenye hoteli moja mjini Mogadishu.

Shambulio hilo ambalo lilianza Ijumaa jioni, lilikuwa ndilo kubwa zaidi kukumba mji mkuu wa Somalia tangu Mohamud aingie madarakani mwezi Juni na kusisitiza changamoto ya kujaribu kumaliza uasi wa miaka 15 wa kundi lenye uhusiano na Al-Qeada.

Watu 21 walifariki na wengine 117 kujeruhiwa katika shambulio hilo la bunduki na mabomu lililolenga hoteli maarufu ya Hayat, na raia wa Norway ni miongoni mwa waliokufa, kwa mujibu wa serikali ya Norway.

“Ninajua kwamba wanainchi wa Somalia wamechoshwa na rambirambi na maombolezo yasiyoisha, najua kwamba mnawapoteza watu wenye thamani katika kila shambulio linolafanywa na magaidi,” Mohamud amesema.

“Tuna dhamira ya kuwadhoofisha magaidi wanaoteketeza wanainchi wetu hadi maeneo yote wanayoyadhibiti yamekombolewa, hili ni jambo la kipaumbele kwa serikali yetu na maandalizi na utelekelezaji wa mpango huo unaendelea,” amesema bila kufafanua zaidi.

XS
SM
MD
LG