Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 25, 2025 Local time: 03:55

Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio aongoza katika hesabu ya kura

Rais wa Sierra Leone na mgombea wa chama tawala Julius Maada Bio akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupiga kura yake kwa ajili ya uchaguzi wa kitaifa katika kituo cha kupigia kura mjini Freetown, Sierra Leone, Juni 24, 2023.

Bio mwenye umri wa miaka 59, anawania muhula wa pili dhidi ya wapinzani 12. Mpinzani wake mkubwa ni mgombea wa All People's Congress (APC) Samura Kamara, ambaye alishindwa kwa kura chache na Bio katika uchaguzi uliopita wa 2018.

Karatasi ya matokeo ya awali ilionyesha Bio amepata zaidi ya kura milioni 1 kufikia sasa, ikilinganishwa na chini kidogo ya laki 8 za Kamara. Matokeo ya mwisho yaliyothibitishwa yatatangazwa ndani ya saa 48 zijazo, tume hiyo ilisema Jumatatu mchana.

Forum

XS
SM
MD
LG