Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 29, 2023 Local time: 20:11

Rais wa Senegal na mwenyekiti wa AU aisihi Ukraine kutegua mabomu ya ardhini kurahisisha usafirishaji wa nafaka


Rais wa Senegal na mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Macky Sall akikutana na Rais wa Russia Vladimir Putin ikulu ya Russia, huko Sochi, June 3, 2022, Picha ya Reuters

Rais wa Senegal na mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Macky Sall Alhamisi ameisihi Ukraine kutegua mabomu ya ardhini kwenye maji ya bahari kando na bandari ya Odesa, ili kurahisisha usafirishaji wa nafaka zinazohitajika kutoka nchi hiyo inayokumbwa na vita.

Uvamizi wa Russia dhidi ya Ukaine na vikwazo vya nchi za magharibi dhidi ya Russia vilikwamisha usambazaji wa nafaka kutoka nchi hizo mbili, na kuzua hofu ya njaa kote ulimwenguni.

Bei ya nafaka barani Afrika, ilipanda kwa sababu ya kukwama kwa usafarishaji wa bidhaa hiyo, na hivyo kuongeza athari za mizozo na mabadiliko ya hali ya hewa na kuzua hofu ya machafuko ya kijamii.

Ikiwa usafirishaji wa ngano kutoka Ukraine hatuanzishwa, Afrika “ itakuwa katika hali ya njaa kali sana ambayo itavuruga usalama wa bara hilo,” Sall ameviambia vyombo vya habari vya ufaransa France 24 na RFI.

Russia na Ukraine zinazalisha asilimia 30 ya ngano yote ya dunia.

Moscow iliiomba Ukraine kutegua mabomu ya ardhini kwenye maji yanayozunguka bandari ya Odesa inayodhibitiwa na Ukraine ili kuruhusu usafirishaji wa nafaka, lakini Ukraine ilikataa kwa kuhofia shambulio la Russia.

Sall amesema Rais wa Russia Vladimir Putin ambaye alikutana naye wiki iliyopita nchini Russia, alimuhakikishia kwamba hilo halitatokea.

“Nilimwambia, Waukraine wanasema hata wakitegua mabomu, utaingia kwenye bandari. Alisema hapana, sitaingia, na hiyo ni ahadi aliyotoa,” rais wa Senegal amesema.

Sall anakutana na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron leo Ijumaa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG