Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 03, 2023 Local time: 20:16

Rais wa Pakistan akataa kutia saini miswaada miwili ya usalama wa taifa


Rais wa Pakistan Arif Alvi

Rais wa Pakistan Arif Alvi Jumapili amesema alikataa kutia saini miswaada miwili kuwa sheria ambayo itatoa mamlaka zaidi ya kuwafungulia mashtaka watu kwa vitendo vya kuipinga serikali na jeshi, hatua ambayo wizara ya sheria imesema ni kinyume cha katiba.

Miswaada hiyo miwili tayari ilipitishwa na mabaraza yote mawili ya bunge la Pakistan lakini Alvi ni mwanachama wa chama cha waziri mkuu wa zamani Imran Khan cha Pakistan Tehreek-e-Insaf(PTI) ambacho kinapinga serikali ya muungano iliyopitisha miswaada hiyo miwili.

“Mungu kama shahidi wangu, sikutia saini mswaada wa marekebisho ya sheria ya siri na mswaada wa marekebisho ya sheria ya jeshi ya mwaka 2023 kwa sababu sikubaliani na sheria hizi,” Alvi alisema kwenye mtandao wa X, ambao zamani ulijulikana kama Twitter.

Amesema aliwaomba wafanyakazi wake kurejesha bungeni miswaada hiyo ambayo haijasainiwa ndani ya muda uliopangwa na kuifanya isifanye kazi.

Forum

​
XS
SM
MD
LG