Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 09:38

Rais wa Nigeria atembelea jimbo la Borno


Wanamgambo wa kimila wakiwa katika kambi moja Maiduguri wakijitolea kulisaka kundi la Boko Haram
Wanamgambo wa kimila wakiwa katika kambi moja Maiduguri wakijitolea kulisaka kundi la Boko Haram

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan alifanya ziara ya kushtukiza kwenda jimbo la Borno lililopo kaskazini mashariki mwa nchi ambako ni kiini cha uasi wa kundi la Boko Haram.

Bwana Jonathan ambaye anafanya kampeni za kuchaguliwa tena alisafiri kuelekea mji mkuu wa jimbo hilo Maiduguri hapo alhamis. Huko alizungumza na wanajeshi kwenye kambi za jeshi na alikutana na mamia ya raia waliokoseshwa makazi kutoka Baga, mji uliotekwa na waasi mwanzoni mwa mwezi huu.

Wakosoaji wa serikali wakitaka juhudi zaidi zifanywe dhidi ya Boko Haram
Wakosoaji wa serikali wakitaka juhudi zaidi zifanywe dhidi ya Boko Haram

Rais amekuwa akikosolewa kwa kutofanya vya kutosha kuwarudisha nyuma waasi au kuwapata zaidi ya wasichana wa shule 200 waliotekwa na kundi la Boko Haram mwezi April mwaka jana. Kundi hilo limeuwa maelfu ya watu na kuteka maeneo mengi ya jimbo la Borno licha ya hali ya dharura iliyotangazwa na bwana Jonathan huko na katika majimbo mawili ya jirani mwezi mei mwaka 2013.

Awali waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry alisema mashambulizi ya karibuni ya Boko Haram huko kaskazini-mashariki mwa Nigeria hayana tofauti na uhalifu dhidi ya binadamu. Kerry alizungumza alhamis wakati wa ziara yake nchini Bulgaria baada ya Amnesty International kutoa picha za satelaiti zilizoonesha uharibifu mkubwa uliosababishwa na wapiganaji wa kundi la Boko haram huko Baga na mji mmoja wa jirani.

Bwana Kerry pia alisema alizungumza na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, Phillip Hammond juu ya juhudi zinazowezekana huko Nigeria kukabiliana na kundi la Boko Haram lakini hakutoa maelezo ya kina.

XS
SM
MD
LG