Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Agosti 17, 2022 Local time: 11:40

Rais wa mpito wa Mali ashambuliwa msikitini


Rais wa mpito wa Mali, Assimi Goita, akiwa na majaji wa mahakama yan juu wakati wa kuapishwa kwake mjini Bamako (Juni 7, 2021)

Wanaume wawili wenye silaha, akiwemo mmoja ambaye alikuwa na kisu, walimshambulia rais wa mpito wa Mali Assimi Goita Jumanne kwenye msikiti wa Great Mosque katika mji mkuu wa Bamako,

Wanaume wawili wenye silaha, akiwemo mmoja ambaye alikuwa na kisu, walimshambulia rais wa mpito wa Mali Assimi Goita Jumanne kwenye msikiti wa Great Mosque katika mji mkuu wa Bamako, mwandishi wa habari wa AFP alishuhudia.

Shambulio hilo lilitokea wakati wa ibada za sherehe za Eid al-Adha.

Goita amechukuliwa kutoka eneo la tukio, kulingana na mwandishi wa habari, ambaye alisema haikufahamika mara moja ikiwa alikuwa amejeruhiwa.

Waziri wa Maswala ya Kidini Mamadou Kone aliiambia AFP kwamba mtu mmoja alikuwa amejaribu kumuua rais kwa kisu lakini alikamatwa.

Latus Toure, mkurugenzi wa Msikiti Mkuu, alisema mshambuliaji alikuwa amemkimbilia rais lakini alimjeruhi mtu mwingine.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG