Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 11, 2025 Local time: 02:36

Rais wa Moldova Sandu atembelea Kyiv kwa mazungumzo na rais Zelenskyy


Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, kulia, akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari na Rais wa Moldova Maia Sandu mjini Kyiv, Ukrainia, Jumamosi, Januari 25, 2025. (AP)
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, kulia, akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari na Rais wa Moldova Maia Sandu mjini Kyiv, Ukrainia, Jumamosi, Januari 25, 2025. (AP)

Rais wa Moldova Maia Sandu aliitembelea Kyiv Jumamosi kwa mazungumzo na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy huku mivutano inaoongezeka huko Transnistria, eneo linaloliunga mkono Russia kutaka kujitenga la Moldova ambalo ni jirani na Ukraine.

Rais wa Moldova Maia Sandu aliitembelea Kyiv leo Jumamosi kwa mazungumzo na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy huku mivutano inaoongezeka huko Transnistria, eneo linaloliunga mkono Russia kutaka kujitenga la Moldova ambalo ni jirani na Ukraine.

Eneo hilo, ambalo lina wakazi nusu milioni, limeshuhudia kukatika kwa umeme tangu mwanzoni mwa mwaka huu kwa sababu mkataba wa usafirishaji gesi wa Kyiv-Moscow ambao uliruhusu gesi ya Russia kwenda huko umeisha.

Kulikuwa na maandamano huko Transnistria siku ya Ijumaa kutoa wito kwa Moldova kuwezesha usafirishaji wa gesi ya Russia na kumaliza shida ya nishati, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.

Forum

XS
SM
MD
LG