Hossam Moniss, alihukumiwa kifungo cha miaka minne jela mwezi Novemba kwa shtaka la kusambaza habari za uongo, shtaka linalotumiwa mara nyingi dhidi ya wapinzani nchini Mistri.
Vyombo vya habari vya ndani vimeripoti kusamehewa kwa Moniss jana Jumatano, wakati wakili Tarek al-Awady na mjumbe wa kamati ya msamaha ya Rais iliyoundwa hivi karibuni, kuandika kwenye Twitter “ hongera, Hossam Moniss amesamehewa.”
Wizara ya mambo ya ndani imesema baadaye katika taarifa kwamba wafungwa 3,273 waliokutwa na hatia katika kesi za uhalifu wamepata msamaha wa rais.
Moniss alikamatwa mwaka wa 2019 pamoja na baadhi ya wabunge wa upinzani waliokuwa wanajiandaa kugombea kwenye uchaguzi wa bunge mwaka wa 2020, chini ya kundi la ushirika “Hope Coalition”.