Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 21:14

Rais wa Mexico aambukizwa Covid kwa mara ya tatu


Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador.

Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador Jumapili amesema kwamba ameambukizwa virusi vya Covid 19 kwa mara ya tatu, akiongeza kuwa ingawa haumwi sana atachukua likizo ya siku chache.

Lopez Obrador, mwenye umri wa miaka 69, ambaye alipata mshtuko mbaya wa moyo mwaka 2013, alionyesha dalili za kawaida alipoambukizwa Covid mara mbili hapo awali wakati janga hilo lilikuwa limekithiri.

Aliandika kwenye akaunti yake ya Twitter “ Sio hatari”. “Moyo wangu unafanya kazi kwa asilimia 100.”

Lopez Obrador amesema waziri wa mambo ya ndani Adan Augusto Lopez ataendesha mikutano yake ya mara kwa mara asubuhi na waandishi wa habari.

Mwezi Januari mwaka 2022, Lopez Obrador aliwekewa kifaa cha kuusaidia moyo wake kufanya kazi vizuri na alionekana ni mwenye afya njema.

XS
SM
MD
LG