Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 05:40

Rais wa Marekani kuadhimisha miaka mia moja ya Mauaji ya halaiki huko Tulsa


Rais wa Marekani Joe Biden akitoa hotuba huko Virginia.
Rais wa Marekani Joe Biden akitoa hotuba huko Virginia.

Rais wa Marekani Joe Biden siku ya Jumanne ataelekea huko Tulsa, Oklahoma kuadhimisha miaka mia moja ya Mauaji ya halaiki ya huko Tulsa, genge la wazungu lilifanya uhariibifu mwaka 1921 lilivamia jamii ya Weusi na kuuwa watu wapatao 300 na kuacha wengine 10,000 wakiwa hawana makazi.

Hadi leo, ni kipindi katika historia ya Marekani juu ya ghasia za rangi ambapo Wamarekani wengi wana ufahamu mdogo, hata wakati nchi inakabiliana na ubaguzi wa siku hizi kukabiliana na shutuma za manyanyaso ya polisi kwa makundi ya wachache, ukosefu wa usawa wa kiuchumi na mijadala mikali juu ya masharti mapya ya upigaji kura ambayo wakosoaji wanasema yanalenga kuzuia kuibuka kwa wapiga kura weusi na Wahispania ili kupunguza ushawishi wao.

Inaelekea kuna watu watatu tu, waliosalia wote wenye umri wa miaka mia moja, kwa jamii ya watu weusi waliokuwa na mafanikio huko Tulsa waliojulikana kama Black Wall Street. Shambulio hilo la kibaguzi lilitokea miongo minne kabla ya Harakati za Haki za Kiraia za mara kwa mara za miaka ya 1960 ambazo zilipelekea haki za kupiga kura kwa Wamarekani Weusi hata wakati mjadala unaendelea sasa juu ya upatikanaji wa haki ya upigaji kura.

XS
SM
MD
LG