Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 08:56

Rais wa Malawi ampokonya mamlaka yote makamu wake kufuatia kashfa ya ufisadi


Rais wa Malawi Lazarius Chakwera akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, kando na mkutano wa kimataifa wa uchumi mjini Davos, Uswiss, May 25, 2022. Picha ya AFP
Rais wa Malawi Lazarius Chakwera akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, kando na mkutano wa kimataifa wa uchumi mjini Davos, Uswiss, May 25, 2022. Picha ya AFP

Rais wa Malawi Lazarius Chakwera Jumanne amempokanya mamlaka yote makamu wake Saulos Chilima baada ya kiongozi huyo kutajwa katika kashfa ya ufisadi iliyoisisimua nchi hiyo.

Uchunguzi ulioendeshwa na taasisi ya kupambana na ufisadi (ACB) kuhusu undanganyifu wa zabuni umehitimisha kuwa maafisa wa umma 53 wa sasa na wa zamani walipokea pesa kutoka kwa mfanyabiashara raia wa Uingereza mwenye asili ya Malawi Zuneth Sattar, kati ya mwezi Machi na Oktoba 2021, Chakwera amesema.

Sattar anafanyiwa uchunguzi nchini Uingereza na Malawi juu ya tuhuma za ufisadi, udanganyifu na utakatishaji wa fedha.

Kulingana na katiba ya Malawi, Chakwera hawezi kumsimamisha kazi au kumfukuza kazi Chilima kwa sababu ni afisa aliyechaguliwa.

β€œLa muhimu nachoweza kufanya kwa sasa, ni kumuweka kando na kumpokonya makujumu yote wakati nikisubiri taasisi ya kupambana na ufisadi ithibitishe tuhuma zinazomkabili,” amesema Chakwera.

Chilima hakutoa maelezo mara moja juu ya uamuzi huo. Alishirikiana na Chakwera kushinda uchaguzi wa rais wa 2020 katika muungano wa kupambana na ufisadi.

Katika hotuba kwa taifa, Chakwera alimfukuza kazi pia mkuu wa polisi George Kainja, ambaye alisikika kwenye mkanda uliorikodiwa akijadili mikataba na Sattar.

​
XS
SM
MD
LG