Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 01, 2022 Local time: 02:05

Rais wa Malawi ameapa kuwafikisha mbaroni waliohusika na rushwa bila huruma


Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera, Lilongwe, Malawi, June 28, 2020.

Rais Chakwera alisema kiwango cha ubadhirifu ni kibaya kuliko kashfa ya rushwa ya mwaka 2013 iliyojulikana kama Cash Gate ambapo fedha za serikali ziliibiwa

Rais mpya wa Malawi, Lazarus Chakwera alisema zaidi ya dola bilioni moja zimeibiwa kwa njia ya rushwa wakati wa utawala wa Rais wa zamani, Peter Mutharika. Katika hotuba yake kwa taifa mwishoni mwa wiki, Chakwera alisema ufujaji huo umebainika katika ripoti ya karibuni ya Mkaguzi Mkuu ambayo iliangalia jinsi serikali ilivyosimamia fedha zake kwa muda wa miaka miwili iliyopita. Chakwera ameapa kuwatia mbaroni waliohusika na rushwa bila ya huruma.

Rais Chakwera alisema, miongoni mwa mambo mengine, ripoti imeonyesha kwamba dola milioni 10 hazikuweza kuelezewa matumizi yake, dola milioni moja zilitumiwa kulipia miradi ambayo haijakamilika na dola laki nne ambazo zilitumiwa kwa mafuta ya petroli bila ya kuwepo kwa nyaraka za matumizi.

Chakwera amesema serikali yake haitakuwa na huruma kwa wale ambao walihusika katika kufanya ubadhirifu wa fedha za serikali.

“Ingawaje awali nilisema kwamba wale waliohusika na ubadhirifu ni vyema wazirudishe hizo fedha, kwa kufanya hivyo haitoshi, kwasababu kiwango cha fedha za walipa kodi ambacho kimeibiwa ni kikubwa mno. Kwahiyo ni makosa kusema kwamba wale waliohusika ni vyema wasamehewe”.

Rais Chakwera alisema kiwango cha ubadhirifu ni kibaya zaidi kuliko kashfa ya rushwa ya mwaka 2013 iliyojulikana kama Cash Gate ambapo kiasi cha dola milioni 32 fedha za serikali ziliibiwa kupitia kandarasi hewa wakati wa utawala wa Rais wa zamani, Joyce Banda.

Chakwera amesema tayari amemuamuru waziri wa sheria kujadili suala hilo la vyombo husika kama kikosi cha kupambana na rushwa katika jeshi la polisi la Malawi na mahakama ili kuharakisha kesi za wizi na rushwa. Hili alisema, linajumuisha kufuatilia mapato yote ya wafanyakazi wa serikali dhidi ya utajiri walio nao.

Hata hivyo Mutharika amekana kuhusika katika kupokea simenti ambayo haikulipiwa ushuru na hivyo kupingana na kauli ya msemaji wake Mgeme Kalirani ambaye aliliambia gazeti moja nchini humo mwezi June kwamba Mutharika anastahili kuagiza bidhaa nje bila ya kulipia kodi.

Baadhi ya wachambuzi wanaiona taarifa ya Mutharika kama mpango wa kukwepa kukamatwa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG